Maendeleo Bank LTD

Sorry! This page is at the moment only in Kiswahili available. We are working on this.


Nunua Hisa uwe Mwanzilishi na Mmiliki


Benki ya Dayosisi – KKKT:DMP

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani limefika katika hatua nzuri sasa kuanzisha Benki, itakayotoa huduma za kibenki kwa wananchi. Hii ni njia mojawapo ya kuuimarisha uchumi wa mtu binafsi, kutegemeza kanisa katika ngazi mbalimbali na kusaidia juhudi za serikali katika kupambana na umaskini. Benki yetu itaitwa MAENDELEO BANK.

Kusudio hili ni utekelezaji wa agizo la Mkutano Mkuu wa Dayosisi wa 2010, wazo lililoanzishwa katika Mkutano Mkuu wa Dayosisi wa 2008. Halmashauri Kuu ya Dayosisi iliyokutana Februari 2010, ilibariki hatua hizi kuanza, chini ya usimamizi wa Halmashauri ya fedha na Mipango ya Dayosisi.

Maono haya yanatekeleza Mpango Mkakati (Strategic Plan) wa Dayosisi (2008-2012), Lengo Na.2 linasema ‘Kuanzisha na Kuimarisha Miradi ya Kiuchumi na Kijamii, kwa kutumia rasilimali zilizopo ndani na nje ya Dayosisi.’

Utekelezaji wa Mradi

Dayosisi, kwa kupitia Halmashauri ya Fedha na Mipango, imeunda kamati ya wataalamu, inayoratibu uanzishwaji wa benki hii. Kamati hiyo inajumuisha waumini waliobobea katika masuala ya Benki, Biashara, Maendeleo na Sheria. Kamati ipo chini ya Uenyekiti wa Msaidizi wa Askofu Mchungaji GEORGE FUPE.

Ofisi ya Mradi


Mradi wa Maendeleo Bank Ltd.
P.O. Box 837
Luther House, Sokoine Drive
Dar es Salaam

Naftal Nsemwa (0754771107)
William Mlaki (07878808072)
Altemius Millinga (0754376122)
Mgisa Mtebe (0713497654)
Rosemary Mushi (0717190413)

Copyright © 2012 ELCT - Eastern and Coastal Diocese. All Rights Reserved